Habakkuk 3:6-10


6 aAlisimama, akaitikisa dunia;
alitazama, na kuyafanya mataifa yatetemeke.
Milima ya zamani iligeuka mavumbi
na vilima vilivyozeeka vikaanguka.
Njia zake ni za milele.

7 bNiliona watu wa Kushani katika dhiki,
na makazi ya Midiani katika maumivu makali.


8 cEe Bwana, uliikasirikia mito?
Je, ghadhabu yako ilikuwa dhidi ya vijito?
Je, ulighadhibikia bahari
ulipoendesha farasi wako
na magari yako ya ushindi?

9 dUliufunua upinde wako
na kuita mishale mingi.
Uliigawa dunia kwa mito;

10 emilima ilikuona ikatetemeka.
Mafuriko ya maji yakapita huko;
vilindi vilinguruma
na kuinua mawimbi yake juu.

Copyright information for SwhKC